NAFASI ZA AJIRA ZA WATUMISHI WATAALAMU WA AFYA 547
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
TAARIFA KWA UMMA
SERIKALI YATOA KIBALI CHA AJIRA MPYA ZA WATUMISHI WA AFYA
547 CHINI WIZARA YA AFYA.
Dodoma, Jumatano Mei 12, 2021.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (WAMJW), imepata kibali cha ajira 547 kutoka Ofisi ya Rais – UTUMISHI za Wataalamu wa kada mbalimbali za Afya wanaokidhi vigezo vya kuaajiriwa chini ya Wizara ya Afya na Taasisi zake.
Huu ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
Ajira 547 inajumulisha nafasi 473 ambazo zitaratibiwa na WAMJW wakati nafasi 74 zitakaratibiwa na Sekretariati ya ajira. Wataalamu 74 wa kada mbalimbali wataajiriwa katika Maabara Kuu ya Taifa; na wataalamu 473 wa kada mbalimbali wataajiriwa katika Hospitali za Kanda za KCMC, Mbeya,
Bugando na Benjamini Mkapa, Hospitali za Rufaa za Mikoa na vyuo mbalimbali vilivyopo chini ya WAMJW.
Watalaamu 473 chini ya uratibu wa WAMJW ambao watanufaika na nafasi hizi ni pamoja na; Madaktari wauguzi, Wafamasia, Wateknolojia wa Dawa, Wateknolojia wa Maabara, Wateknolojia wa Mionzi, Wateknolojia wa Macho, Watoa Tiba kwa Vitendo, Maafisa Afya Mazingira, Wasaidizi wa
Ajira hizo (473) zitajaza nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliokoma utumishi kutokana na sababu mbalimbali. Waombaji wanasisitizwa kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na vyanzo rasmi vya taarifa za ajira na utaratibu kupitia tovuti www.moh.go.tz kwa kiunganishi (ajira.moh.go.tz). Maombi ni kuanzia tarehe 12 hadi 25 Mei, 2021.
No comments