TANGAZO LA KAZI WIZARA YA FEDHA NA KALIUA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/L/101 10 Mei, 2021
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara ya
Fedha na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi mbili (02) kama zilivyoainishwa
katika tangazo hili.
1.0 MWAJIRI: WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO NA HALMASHAURI YA WILAYA
YA KALIUA.
1.0.1 MSAIDIZI WA HESABU DARAJA LA II - (NAFASI 02)
1.0.2 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kuandika na kutunza Regista zinazohusu shughuli za uhasibu;
ii. Kutunza kumbukumbu za hesabu;
iii. Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki; na
iv. Kufanya kazi nyingine za fani yake atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
1.0.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti cha Astashahada ya Uhasibu kutoka chuo kinachotambuliwa na
Serikali au cheti cha ATEC I kinachotolewa na NBAA au sifa nyingine zinazolingana na
hizo zinazotambuliwa na NBAA.
1.0.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B.
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za
kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za
maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe
ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V)
yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya
wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti
vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na
vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective
boards)
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati
matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS
SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na
NACTE).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko
katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
3 yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 24, Mei, 2021. Muhimu, kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P. 2320 DODOMA.
i. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/
(Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
ii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
Limetolewa na;
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
No comments