Breking New

TANGAZO LA KUITWA KAZINI AJIRA ZA MKATABA KUPITIA UFADHILI WA GLOBAL FUND, IVD/GAVI NA CDC/PEPFAR





1. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya) inapenda kuwataarifu waombaji wa ajira za Mikataba kupitia ufadhili wa Miradi ya Global Fund na IVD/GAVI waliofanya usaili tarehe 8 22 Machi, 2021 na Mradi wa CDC/PEPFAR waliofanya usaili tarehe 23-25 Machi, 2021 na ambao wamefaulu usaili huo wanaitwa kazini. 

2. Wote waliofaulu na ambao majina yao yameorodheshwa kwenye tangazo hili wanatakiwa kuripoti (Mara moja) katika Ofisi za Wizara katika jengo la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya tarehe 17 Mei, 2021, ghorofa ya nne kwa ajili ya kujaza Mkataba wa ajira wakiwa na nakala mbili (2) kwa kila cheti ambacho kilitumika wakati wa kuomba ajira na katika usaili ikiwa ni pamoja na; 

a) Nakala ya cheti cha kuzaliwa; 

b) Nakala ya vyeti vya elimu ya Sekondari (Kidato cha Nne na Sita); 

c) Nakala ya vyeti vya taaluma; 

d) Nakala ya Cheti cha Mafunzo kwa Vitendo (Internship); 

e) Nakala ya Cheti cha usajili kutoka Baraza husika (Valid Licence); 

f) Nakala ya Ithibati ya vyeti vya elimu na taaluma (Accreditation na Equivalence) kutoka TCU na NECTA kwa wale waliosoma vyuo nje ya nchi pamoja na wale waliosoma Sekondari nje ya nchi/Mitaala ya nje; 

g) Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako pamoja na cheti cha kuzaliwa hakikisha unawasilisha kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa Viapo na Kusajiliwa na Msajili wa Hati, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi; 

h) Nakala ya Kitambulisho/namba ya Uraia (NIDA); na 

i) Picha mbili (2) Passport Size. Aidha, yeyote atakayeripoti na ‘Transcript’ tu au kuwa na nakala pungufu ya vielelezo tajwa hapo juu hatapokelewa. 

3. Waombaji wote ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili wafahamu kuwa hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba tena wakati nafasi za kazi zitakapotangazwa.



No comments