TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI TARI NA WIZARA YA MIFUGO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Kumb.Na.EA.7/96/01/L/122 26 Mei, 2021
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) na Wizara ya Mifugo na Uvuvi anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi nne (4) kama zilivyoainishwa katika tangazo hili;-
1.0 MWAJIRI: TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA (TARI)
1.0.1 AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA III – NAFASI 03
1.0.2 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kushirikiana na Wakulima kuendesha mashamba ya majaribio na mashamba darasa;
ii. Kutembelea Wakulima/vikundi vya Wakulima katika mashamba yao na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya mbinu bora na za kisasa za kilimo cha kibiashara;
iii. Kufundisha na kuwaeleza Wakulima juu ya matumizi bora ya mbolea, madawa na zana za kilimo;
iv. Kukusanya na kutunza takwimu za hali ya kilimo katika Kijiji;
v. Kubuni na kuandaa vihenge vya kisasa vya hifadhi ya mazao na kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mazao;
vi. Kutoa taarifa juu ya dalili za kuwepo visumbufu vya mimea na mazao;
vii. Kuandaa na kutumia daftari la kilimo katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku;
viii. Kushiriki katika mchakato wa kuibua fursa na vikwazo vya maendeleo na kuandaa Mpango wa Maendeleo ya Kilimo wa kijiji;
na
ix. Kuandaa taarifa ya utekelezaji ya kila mwezi na kuiwasilisha kwa Afisa Ugani wa kata na nakala kuiwasilisha kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji.
1.0.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne (IV) wenye Astashahada ya Kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
1.0.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B.
2.0 MWAJIRI: KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI
2.0.1 MHUDUMU WA BOTI – NAFASI 1 (INARUDIWA)
2.0.2 MAJUKUMU YA KAZI
i. Kulinda Boti/Meli;
ii. Kutunza usafi wa Meli/Boti;
iii. Kutunza usafi wa vyombo vya kuvulia samaki;
iv. Kufanya ukarabati mdogo wa Meli/Boti ya uvuvi; na
v. Kuegesha boti dogo la uvuvi kama inavyotakiwa.
2.0.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne (IV) wenye cheti cha uvuvi kutoka Chuo cha Uvuvi Nyegezi au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
2.0.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS A kwa mwezi.
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE.
i. Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazihusika.
- Postgraduate/Degree/AdvancedDiploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii.Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao
vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA naNACTE).
viii.Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix.Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
x.Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xi.Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 08, Juni, 2021. Muhimu: kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu na itumwe kwa;
KATIBU OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P. 2320 DODOMA.
xii.Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).
xiii.Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
IMETOLEWA NA; KATIBU SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
No comments