Huu Hapa Ushauri wa Kocha Gomes kwa Uongozi wa Simba
Kocha mkuu wa klabu ya Simba Didier Gomes ameishauri Bodi ya wakurungezi ya Simba kuwa kutokana na ligi ya Tanzania kuchelewa kuisha amewaomba baada ya fainali ya kombe la shirikisho (ASFC) dhidi ya Yanga July 25 wachezaji wapewa mapumziko ya wiki moja na August 01 warudi kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao (2021/22)
Gomes amedai kuwa mashindano ya CAF Champion League yataanza mwanzoni mwa mwezi September hivyo anataka kupata muda wa mwezi mzima kuandaa kikosi chake kwa ajili ya mashindano hayo pia ameutaka uongozi huo kutobadili sana kikosi kwa sababu wanaweza wakaanza upya na yasijirudie ya msimu wa 2019/20 ya kutolewa mapema.
Uongozi wa Bodi ya klabu ya Simba umebariki ratiba hiyo na kwa sasa unakamilisha usajili wa wachezaji 5 wapya ikiwa 3 wa ndani (ambao tayari) na 2 wa kimataifa (ambao wapo mbioni kukamilisha) na uongozi umesema kambi ya maandalizi ya msimu ujao itakuwa nchini Misri na wameshapanga tayari na michezo ya kirafiki na timu kubwa za Misri kama Al Ahly.
No comments