NAFASI ZA KAZI MLIMBA DC
1.0 MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA III – NAFASI 5.
1.1 SIFA ZA MWOMBAJI:-
1.Awe na Elimu ya Kidato cha Nne/ Sita2.Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada/ Cheti NTA LEVEL 5 katika moja ya fani zifuatazo.
- Utawala
- Rasilimali watu
- Sheria
- Maendeleo ya Jamii
- Elimu ya Jamii
- Usimamizi wa fedha au
- Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa naSerikali
4. Awe amesajiliwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) mwenye kadi au namba ya usajili wa NIDA
1.2NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia Viwango vya Serikali kwa ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi1.3 MAJUKUMU YA KAZI
- Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
- Kusimamia Ulinzi na Usalama wa raia na mali zao, kuwa mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
- Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Kijiji
- Kuratibu Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji
- Kutafsiri na Kusimamia Sera, Sheria na taratibu za uendeshaji wa Serikali ya Kijiji
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji
1.4 MASHARTI YA JUMLA
- Awe Raia wa Tanzania
- “Testimonials Provisional Results, Statement of Result” na hati za matokeo kidato cha Nne na Sita (Form IV na VI na Result Slips) HAVITAKUBALIWA
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimekaguliwa na kuthibitishwa na mamlaka husika (NECTA, NACTE NA TCU)
- Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
1.5NAMNA YA KUTUMA MAOMBI;-
Kila muombaji wa kazi awasilishe barua ikiambatishwa na;-- Wasifu Binafsi (CV)
- Vivuli vya Vyeti Elimu na Ujuzi
- Cheti cha Kuzaliwa
- Picha mbili za “Passport Size”
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P 263,
IFAKARA
1.7 Mwisho wa kupokea Maombi ni tarehe 26/07/2021 siku ya Jumatatu ,saa 9.30 alasiri.TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI MLIMBA DC 14-07-2021
No comments