Breking New

NAFASI ZA KAZI (UTUMISHI) HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA

 


TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WENYE SIFA NA NIA YA KUFANYA KAZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA NAFASI MBALIMBALI ZA KAZI KAMA IFUATAVYO

1. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA I1. NAFASI [3]

SIFA ZA MWOMBAJI:

  • Awe amehitimu Kidato cha Nne au sita
  • Awe amehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani zifuatazo:-Utaiwala,Shenia, Elimu ya Jami, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamil na Sayansi ya Jamil kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikal.

MAJUKUMU YAKE:

  • Kuwa Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijjl.
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa Raia na Mali zao.
  • Kuratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa mipango ya Maendeleo ya Kijij.
  • Kuwa katibu wa mikutano yote ya Halmashauri ya Kijj.
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu.
  • Kusimamia, Kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijij.

NGAZI YA MSHAHARA TGS B


2. MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II. NAFASI (3)

SIFA ZA MWOMBAJI:

  • Awe amehitimu kidato cha nne au sita mwenye cheti cha utunzaji wa kumbukumbu katika mojawapo ya fani za Afya, Masjala, Mahakama na Ardhi.

MAJUKUMU YAKE:

  • Kutafuta kumbukumbu/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji
  • Kudhibiti upokeaj, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
  • Kuchambua, kuorodhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi kulingana na
  • somo husika (Classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
  • Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (File racks/cabinets) katika
  • masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
  • Kuweka kumbukumbu (barua Nyaraka nk) katika mafaili
  • Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/ nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA TGS B

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WA KAZI ZOTE.

  1. Mwombaji awe ni Raia wa Tanzania
  2. Awe na umri usiozidi miaka miaka 45 na usiopungua miaka 18
  3. Maombi yote yaambatishwe na nakala ya cheti cha Taaluma, cheti cha Kidato cha Nne na cheti cha kuzaliwa
  4. Maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV) ikiwa na anuani, namba za simu za kuaminika majina matatu ya wadhamini na picha mbili (Passport Size) za hivi karibuni
  5. Vyeti vyote vya Taaluma, Kidato cha Nne na cheti cha kuzaliwa vithibitishwe na Hakimu/Wakili anayetambulika na Serikali
  6. Aidha, uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za Kisheria na Mamlaka zinazohusika
  7. Testimonial results, statement of results na hati za matokeo ya Kidato cha Nne/Sita (Form IV na Form VI result slip) havitakubalika
  8. Watumishi waliopunguzwa kazi/kufukuzwa kazi Serikalini hawaruhusiwi kuomba
  9. Mwombaji yeyote ambaye hatazingatia mojawapo ya masharti au vigezo tajwa hapo ju maombi yake hayatashughulikiwa
  10. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi ilyoandikwa kwa Kiswahilli /Kiingereza na barua hiyo ielekezwe kwa

Mkurugenzi Mtendaji (W)

Halmashauri ya Wilaya ya Iringa

S.L.P. 10p8

IRINGA

Mwisho wa kupokea maombi ya kazi ni tarehe 06 Agosti, 2021.

news TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI IRINGA DC

No comments