TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI TAASISI MBALIMBALI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Maji, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Fedha na Mipango, Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD), Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Maabara ya Taifa (NHL) na Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Taasisi ya Uvuvi wa Samaki Tanzania (TAFIRI), Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu katika Ukanda wa Kitropiki (TPRI), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) na Halmashauri ya Wilaya ya Nzega. anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 23 – 29 Julai, 2021 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
- Usaili utafanyika kuanzia tarehe 23 – 29 Julai, 2021 kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili; muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
- Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask);
- Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
- Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
- Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
- Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
- Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi;
- Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
- Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA);
- Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
- Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
- Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili
No comments