Billnass na Nandy ndio 'bai bai'? Billnass aonesha familia yake mpya
Rapa kutoka nchini Tanzania Billnass ametikisa kiwanda cha burudani kwa mara nyingine baada ya kumuonesha mtoto wake hadharani.
Rapa huyo ambaye anatamba na wimbo wake wa "Tatizo", kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye wafuasi Milioni 3.5 alichapisha picha akiwa amebeba mtoto huku pembeni akiwa na mwanadada na kisha kusindikiza picha hiyo na ujumbe "La familia Nengatronix"
Watu wengi wameendelea kubaki na maswali kama huyo ni mtoto wa 'Nenga' kwani yeye binafsi kando na kuchapisha picha hiyo bado hajaweka wazi kuthibitisha tetesi hayo kwani akiwa anafanya mahojiano na Lil Ommy wiki chache nyuma msanii huyo alisema kuwa yeye hana mtoto.
Hii si mara ya kwanza kwa 'Nenga' kupost mtoto kwenye akaunti yake ya Instagram kwani siku sita zilizopita pia alichapisha picha akiwa amebeba mtoto na kuandika"Nengatronix" na hivyo kuzua mjadala mkubwa sana kwenye mitandao ya kijamii.
Ikumbukwe kuwa miezi michache iliyopita Billnass alikuwa kwenye mahusiano na mwanamuziki Nandy ila kwa siku hivi karibuni wawili hao hawajaonekana wakiwa pamoja na wawili hao hawajathibitisha kuwa bado wako kwenye mahusiano au lah.
Billnass anajulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kurap na kutoa nyimbo zilizotamba ndani na nje ya Tanzania kama "Sina Jambo", "Chafu Pozi", "Mazoea" pamoja na "Tatizo
No comments