MABADILIKO YA USAILI KWA KADA YA PERSONAL SECRETARY II YA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA)
Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawajulisha waombaji kazi wa nafasi ya “Personal Secretary” katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa hakutakuwa na usaili wa mchujo kwa kada ya PERSONAL SECRETARY II uliopangwa kufanyika tarehe 07-08-2021.
Hivyo wanapaswa kujiandaa kwa ajili ya usaili wa Vitendo utakaofanyika tarehe 23-08-2021 saa 1:00 kamili asubuhi katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira Majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Eneo la Dkt.Asha Rose Migiro.
Sekretarieti ya Ajira inawaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwa mabadiliko hayo.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi Umma
04 Agosti, 2021
No comments