Nafasi za kazi za Udereva Halmashauri ya Mji wa Mbinga
DEREVA II (4)
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa waliohitimu kidato cha Nne (Form lV) na leseni ya udereva ya Daraja E au Cl
ya uendeshaji wa magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja
bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari
(Basic Driving Course) yanayotolewa na chuo cha Ufundi Stadi (VETA) au chuo kingine
kinachotambuliwa na serikali. Wombaji wenye cheti cha majaribio ya Ufundi ll
watafikiriwa kwanza.
KAZI NA MAJUKUMU
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
iii. Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
v. Kujaza na kutunza laarifa za safari zote katika daftari la safari
vi. Kufanya usafi wa gari na
vii. Kufanya kazi zingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
No comments