Breking New

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUTHIBITISHA KUJIUNGA NA VYUO VYA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI KWA WALIOCHAGULIWA NA OR-TAMISEMI MWAKA WA MASOMO 2021/202

 




Tarehe 1 Juni, 2021, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (ORTAMISEMI) alitoa taarifa ya wanafunzi waliohitimu kidato cha Nne, 2020 kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi vinavyosimamiwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE). Katika taarifa hiyo, wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi walielekezwa kuthibitisha kukubali nafasi hizo kuanzia tarehe 1 Juni mpaka tarehe 8 Agosti, 2021 kupitia tovuti ya Baraza www.nacte.go.tz kwa kubofya kitufe cha Uthibitisho uchaguzi OR-TAMISEMI 2021.

Hadi kufikia tarehe 31 Julai, 2021 jumla ya wahitimu 25,808 tu kati ya 46,431 waliochaguliwa ndiyo waliothibitisha kujiunga na vyuo mbalimbali, ikiwa ni sawa na asilimia 56.8 ya wanafunzi wote. Baraza linapenda kuwakumbusha na kuwahimiza wanafunzi wote waliochaguliwa na hawajathibitisha kutumia muda huu mchache uliobaki kuthibitisha nafasi zao mpaka tarehe 8 Agosti, 2021 kupitia tovuti ya Baraza www.nacte.go.tz kwa kubofya kitufe cha Uthibitisho uchaguzi OR-TAMISEMI 2021. Aidha, wahitimu ambao hawatathibitisha kujiunga na vyuo walivyoomba watapoteza nafasi zao na hawatakuwa na sifa za kuomba uhamisho endapo watahitaji kufanya hivyo kuanzia tarehe 9 hadi tarehe 23 Agosti 2021 katika Vyuo na Programu zenye nafasi.

Baraza linaomba kila atakayepata taarifa hizi amjulishe na mwenzake. 


No comments