Breking New

Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania msimu wa 2021/2022.

 

MTENDAJI Mkuu wa Bodi ya Ligi ya Tanzania (TPLB) Almas Kasongo ametangaza kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu wa 2021/2022 itaanza September 27,2021.

Kasongo amesema kuwa jumla ya michezo 240 itachezwa na kuonyeshwa mbashara/Live na Azam TV

Aidha Kasongo ameongeza kuwa Ligi itasimama kupisha ratiba ya FIFA/CAF mara 19, Azam Sports Federation Cup na Mapinduzi Cup itafanya kusimama kwa Ligi hiyo pia.

Mechi zitachezwa saa 8 mchana, 10 jioni, 11 jioni 12 jioni, saa moja usiku na saa mbili usiku.

Mechi zitachezwa katikati ya wiki na mwisho wa wiki huku Mchezo wa kwanza wa Derby ya Dar es Salaam kati ya Simba na Yanga ukitarajiwa kupigwa December 11,2021.

Simba na Yanga zitafungua msimu mpya wa Ligi kwa kucheza mchezo wa ngao ya Jamii unaotarajiwa kuchezwa September 25,2021 kabla ya Ligi kuanza rasmi September 27.

Hii ni ratiba ya Michezo ya ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2021/2022.












No comments